Shughuli ya utamaduni wa chai wa China yafanyika Jordan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 03, 2024
Shughuli ya utamaduni wa chai wa China yafanyika Jordan
Mshiriki wa shughuli akijipiga selfie na waigizaji waliovalia mavazi ya kikabila kwenye Kituo cha Utamaduni wa China mjini Amman, Jordan, Juni 30, 2024. (Picha na Mohammad Abu Ghosh/Xinhua)

AMMAN – Shughuli ya kutangaza na kueneza utamaduni wa chai wa China imefanyika Jumapili mjini Amman, Jordan, huku maonyesho ya kuvutia ya muziki na ngoma za kijadi na mavazi ya kikabila yakifanyika na yameonesha sifa za kipekee za Mkoa wa Yunnan, Kusini mwa China.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa shughuli hiyo, Balozi wa China nchini Jordan Chen Chuandong amesema historia ya China ya kutengeneza na kunywa chai ilianzia miaka karibu 5,000 iliyopita, na kuenea kwa chai duniani kumechochea mawasiliano na mafungamano kati ya ustaarabu wa dunia, ikiwa ni pamoja na ustaarabu wa nchi mbalimbali za Kiarabu.

Yang Cheng, naibu mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni na Utalii ya Mkoa wa Yunnan, kwa fahari alitambulisha kwa umma mbinu sita za utengenezaji wa chai na mila na desturi husika za kijamii za mkoa wake, ikiwa ni pamoja na mbinu za jadi za utengenezaji wa chai ya Pu'er na mila na desturi za chai za kabila dogo la Wabai.

Amebainisha kuwa mbinu hizo sita ni sehemu ya "mbinu za jadi za utengenezaji wa chai na desturi zinazohusika za kijamii nchini China" ambazo ziliorodheshwa na UNESCO Mwaka 2022 kuwa mali ya urithi wa utamaduni usioshikika, akielezea matumaini kwamba shughuli hiyo itasaidia kuongeza uelewa wa tamaduni za kikabila za Yunnan kati ya watu wa Jordan na kuhimiza mawasiliano na ushirikiano kati ya Jordan na Yunnan, China katika mambo ya utamaduni.

Shughuli hiyo iliyofanyika kwenye Kituo cha Utamaduni wa China mjini Amman na kuendelea hadi Julai 2, ilishuhudia ufunguzi wake ukivutia washiriki zaidi ya 300 kutoka China, Jordan na nchi nyingine. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha