Dada mkubwa wa mapacha Watatu wa Panda wa Guangzhou, China azaa kitoto (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 03, 2024
Dada mkubwa wa mapacha Watatu wa Panda wa Guangzhou, China azaa kitoto
Kitoto kichanga cha panda kilichozaliwa na panda “Meng Meng” kikipokea upimaji wa afya huko Changlong, Mji wa Guangzhou wa China. (Picha na Liu Dawei/Xinhua)

Miaka 10 iliyopita, mapacha watatu pekee wa panda duniani walizaliwa huko Changlong, Mji wa Guangzhou wa China. Tarehe 18, Juni mwaka huu, dada mkubwa wa mapacha hao aitwaye “Meng Meng”, kwa mafanikio alizaa kitoto kichanga cha kike cha panda. Uzito wa sasa wa kitoto hicho umeongezeka hadi gramu 462 kutoka uzito gramu 178 wa wakati wa kuzaliwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha