Chuo Kikuu cha NPU Tawi la Kazakhstan chaimarisha mawasiliano kati ya China na Kazakhstan katika mambo ya elimu (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 03, 2024
Chuo Kikuu cha NPU Tawi la Kazakhstan chaimarisha mawasiliano kati ya China na Kazakhstan katika mambo ya elimu
Murat, mwanafunzi wa tawi la Kazakhstan la Chuo Kikuu cha Viwanda cha Xibei cha China (NPU) akiazima kitabu kwenye maktaba ya NPU mjini Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini Magharibi mwa China, Juni 26, 2024.

ALMATY - Jengo linalovutia mjini Almaty, Kazakhstan sasa linaonyesha jina "Tawi la Kazakhstan la Chuo Kikuu cha Viwanda cha Xibei cha China” lililoandikwa kwa Lugha za Kikazakh, Kichina na Kiingereza. Hii inaonesha hatua muhimu katika ushirikiano wa elimu kati ya China na Kazakhstan.

Mwezi Mei 2023, wakati wa Mkutano wa Kilele wa China na Nchi za Asia ya Kati, Chuo Kikuu cha Viwanda cha Xibei cha China (NPU) na Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Al-Farabi Kazakh vilitia saini makubaliano ya ushirikiano wa kuanzishwa kwa tawi la Kazakhstan la NPU.

Mwezi Oktoba 2023, muda mfupi tu kabla ya Jukwaa la Tatu la Mkutano wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, tawi la Kazakhstan la chuo kikuu hicho lilifunguliwa rasmi na kukaribisha kundi la kwanza la wanafunzi wake.

Tawi hilo linajikita katika kozi za shahada katika sayansi ya vifaa, sayansi ya kompyuta na teknolojia, na uhandisi wa upashanaji wa habari na mawasiliano ya habari.

Mmoja wa wanafunzi wa kwanza, Bolysbek Murat Yerzhanuly mwenye umri wa miaka 22, anasoma shahada ya uzamili katika sayansi na teknolojia ya kompyuta, akijikita katika ubobezi wa matumizi ya akili bandia (AI) kwenye elimu ya matibabu.

Mapema mwezi wa Juni, Murat na wanafunzi wengine saba walisafiri hadi Xi'an, China, kwa ajili ya tathmini za maandiko ya tasnifu zao katika chuo kikuu cha NPU. Wakati walipokuwa chuoni hapo, walijionea mazingira ya chuo hicho, kutembelea kuta za mji wa kale, na wakachangamana na utamaduni wa wenyeji.

Kwa mwongozo wa maprofesa wao, wanafunzi wote wanane wamekamilisha maandiko yao ya tasnifu.

Kuanzia Septemba, Murat na wanafunzi wenzake wataanza programu ya masomo ya mwaka mmoja katika Mji wa Xi'an. "Xi'an ni mji mzuri, na ninajisikia vizuri sana hapa," Murat amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha