Wapalestina takriban 12 wauawa katika shambulizi la anga la Israel katikati mwa Gaza (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 03, 2024
Wapalestina takriban 12 wauawa katika shambulizi la anga la Israel katikati mwa Gaza
Wapalestina wakiyakimbia maeneo ya mashariki ya Khan Younis, Kusini mwa Ukanda wa Gaza, Julai 2, 2024. (Picha na Rizek Abdeljawad/Xinhua)

GAZA - Wapalestina wasiopungua 12 wameuawa katika shambulizi la anga la Israel lililolenga jengo katika eneo la Deir al-Balah, katikati mwa Ukanda wa Gaza, vyanzo vya habari ndani ya Palestina vimesema siku ya Jumanne ambapo wengine kadhaa waliojeruhiwa wamehamishiwa katika Hospitali ya Al-Aqsa katika mji huo, vyanzo vya matibabu vya Palestina vimeliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.

Hakukuwa na maoni ya mara moja kutoka kwa jeshi la Israeli juu ya tukio hilo.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa siku ya Jumanne, Jeshi la Ulinzi la Israel lilisema linaendelea na operesheni zake katika makazi ya Shejaiya yaliyoko Mji wa Rafah wa kaskazini mwa Gaza, na sehemu ya kati ya Gaza.

Katika kipindi cha saa 24 zilizopita, shambulizi la Israel limesababisha vifo vya watu 25 na wengine 81 kujeruhiwa, na kufanya jumla ya vifo vya Wapalestina huko Gaza kufikia 37,925 na majeruhi kufikia 87,141 tangu mgogoro wa Palestina na Israeli uanze mapema Oktoba 2023, mamlaka ya afya ya Gaza imesema katika taarifa yake siku ya Jumanne.

Israel ilianzisha mashambulizi makubwa dhidi ya Kundi la Wanamgambo wa Hamas katika Ukanda wa Gaza kulipiza kisasi dhidi ya mashambulizi ya kundi hilo kupitia mpaka wa kusini wa Israel tarehe 7 Oktoba 2023, ambapo watu takriban 1,200 waliuawa na zaidi ya 250 kuchukuliwa mateka.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha