Mizigo ya bidhaa inayopita Eneo Maalum la Kimataifa la Usafirishaji wa Bidhaa la SCO Mashariki mwa China yafikia tani milioni 289

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 05, 2024
Mizigo ya bidhaa inayopita Eneo Maalum la Kimataifa la Usafirishaji wa Bidhaa la SCO Mashariki mwa China yafikia tani milioni 289
Picha iliyopigwa Agosti 16, 2023 ikionyesha kreni ya magurudumu ikipakia kontena kwenye treni katika Eneo Maalum la Kimataifa la Usafirishaji wa Bidhaa la SCO (kwenye Bandari ya Lianyungang) la Mji wa Lianyungang, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China. (Picha na Wang Jianmin/Xinhua)

Eneo Maalum la Kimataifa la Usafirishaji wa Bidhaa la Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (kwenye Bandari ya Lianyungang) lililoanzishwa mwaka 2015 ni eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 69.79 , ambapo kuna viwanda zaidi ya 1,600. Eneo hilo limeunda mfumo wa usafirishaji na usambazaji wa pamoja ulio wa kisasa, barabara, reli, mito na bahari, na pia vimeunganishwa kwa viwanda vya raslimali mpya na nishati mpya.

Hadi kufikia mwisho wa Juni mwaka huu, uchukuzi wa jumla wa mizigo wa eneo hilo ulifikia tani milioni 289 ukiwa na mapato ya biashara ya uchukuzi ya yuan bilioni 19.06 (kama dola bilioni 2.62 za U.S.). 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha