Jamii za Botswana zanufaika na utalii wa uwindaji na kupiga picha

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 05, 2024
Jamii za Botswana zanufaika na utalii wa uwindaji na kupiga picha
Watalii wakitazama tembo kwenye mto Chobe wa kijiji cha Kasane, Botswana, Septemba 23, 2022. (Picha na Metlha Ngubevana/Xinhua)

GABORONE - Utalii wa uwindaji na kupiga picha kaskazini mwa Botswana umeleta manufaa ya kifedha na kijamii kwa wenyeji kupitia amana za jamii chini ya mpango wa Usimamizi wa Maliasili wa Jamii (CBNRM), Wizara ya Mazingira na Utalii ya Botswana imesema.

Kupitia utalii wa uwindaji, wanapata mapato, kupata faida kutoka kwa nyama za wanyamapori, kusimamia maliasili zao, na kusambaza faida zao ndani ya jamii, Johane Tlholego Ngwengare, chifu wa Kijiji cha Phuduhudu wilayani Kgalagadi, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano siku ya Jumatano.

Ngwengare amesema, kutokana na kuwa na Taasisi ya Xhauxhwatubi Development Trust kijijini hicho, tembo anapowindwa, taasisi hiyo ina utaratibu wa kusambaza nyama ya pori kwa usawa kati ya familia 153 za kijiji hicho bila malipo.

"Mwishoni mwa mwaka, kila familia katika kijiji inaweza kupokea pula 2,000 (kama dola 150 za Marekani)," amesema.

Mpango wa CBNRM, ulioanza kutekeleza kwa majaribio mwaka 1993 , unalenga kushirikisha jamii zilizo karibu na mbuga za wanyama na hifadhi za wanyama katika uhifadhi wa maliasili, hususan wanyamapori, na kuepusha migogoro kati ya binadamu na wanyamapori.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mazingira na Utalii ya Botswana, mpango wa CBNRM kimsingi unahusisha shughuli za utalii zinazozingatia wanyamapori kama vile utalii wa kupiga picha na uwindaji, lakini pia unatoa fursa kwa jamii za wenyeji kushiriki katika kuendeleza utalii na uhifadhi wa maliasili.

Kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa na Idara ya Wanyamapori na Bustani za Kitaifa ya Botswana, uwindaji kama huo kila mwaka unaleta faida kati ya pula milioni 13 na pula milioni 31 kwa taasisi ya hiyo.

Jamii za kaskazini mwa Botswana, kama zile za vijiji vya Sankoyo, Khwai, na Mababe, zimeacha shughuli za jadi za kujipatia riziki kama uwindaji wa kujikimu, kukusanya mazao ya porini, na kilimo, na kujishughulisha na shughuli za uchumi zinazotegemea fedha taslimu, huku mapato kutoka CBNRM yakiwa chanzo kikuu kwa wao kujikimu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha