Kazi ya kuhamisha wakaazi yatekelezwa baada ya kubomoka kwa lambo la maji katikati ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 08, 2024
Kazi ya kuhamisha wakaazi yatekelezwa baada ya kubomoka kwa lambo la maji katikati ya China
Wakazi waliohamishwa wakiwa wamepumzika kwenye eneo la makazi ya muda lililoko shule ya ufundi stadi katika Wilaya ya Huarong, Mji wa Yueyang, Mkoa wa Hunan, katikati ya China, Julai 7, 2024. (Xinhua/Chen Zhenhai)

Majira ya saa 11:48 jioni siku ya Ijumaa, lambo la Ziwa Dongting lilibomoka katika Mji mdogo wa Tuanzhou, Wilaya ya Huarong, Mji wa Yueyang katika Mkoa wa Hunan, katikati ya China na kusababisha mafuriko katika eneo hilo. Sehemu iliyobomoka hapo awali ilikuwa wa upana wa mita 10 lakini baadaye ilipanuka.

Kufuatia kuhamishwa mara moja kwa wakaazi karibu 5,000 kutoka eneo hilo lililoathiriwa, hatua za haraka zimechukuliwa kukarabati sehemu hizo zilizobomoka. Hadi kufikia Jumapili jioni, sehemu yenye ukubwa wa mita 75 kati ya eneo zima la mita 226 lililobomoka ilikuwa imeshazibwa, kwa mujibu wa makao makuu ya udhibiti wa mafuriko na misaada ya ukame ya Yueyang.

Makao makuu hayo yamesema waokoaji 4,739 wametumwa kwa haraka hadi ilipokuwa imefikia saa 2 usiku jana Jumapili.

Kwa sasa, Wilaya ya Huarong imeanzisha maeneo manne ya kuhamisha na kuwapa waathirika makazi ya muda, na wakazi jumla ya 3,224 walioathiriwa wamehamishwa na kupewa makazi ya muda. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha