Bustani ya ndani ya barafu na theluji ambayo ni kubwa zaidi duniani yafunguliwa Harbin, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 08, 2024
Bustani ya ndani ya barafu na theluji ambayo ni kubwa zaidi duniani yafunguliwa Harbin, China
Watalii wakiburudika kwenye bustani ya ndani ya barafu na theluji huko Harbin, Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, Julai 6, 2024. (Picha na Yin Zhongwei/Xinhua)

Watalii wanaotembelea Harbin, "Mji wa Barafu" wa China ulioko Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini kabisa mwa China, sasa wana kivutio kipya cha kutembelea, ambacho ni bustani ya ndani ya barafu na theluji iliyofunguliwa siku ya Jumamosi.

Ikiwa imejengwa kwenye eneo la ukubwa wa mita za mraba 23,800, bustani hiyo imeshinda Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa kuwa bustani ya ndani ya barafu na theluji ambayo ni kubwa zaidi duniani.

Meneja wa bustani hiyo amesema kuwa kituo hicho kina sehemu tisa zenye maudhui mbalimbali zikionyesha sanamu za barafu zinazoonyesha uhalisia wa maisha ziking'arishwa na mwanga wa rangi mbalimbali. Bustani hiyo hudumisha halijoto isiyobadilika ili kupokea watalii kwa majira ya mwaka mzima.

Bustani hiyo itaenda sambamba na Bustani ya Barafu na Theluji ya Harbin, ambayo ni bustani kinara ya nje ya barafu na theluji inayochukua eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 810,000, na hivyo itaifanya Harbin kuwa kivutio cha mapumziko na utalii kinachofaa majira yote.

Mji wa Harbin wenye majira ya baridi kali unajulikana kwa tamasha lake la kila mwaka la barafu na theluji. Bustani ya Barafu na Theluji ya Harbin ilipokea wastani wa watalii zaidi ya 30,000 kila siku katika majira ya baridi yaliyopita.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha