China yafanya shughuli ya kukumbuka miaka 87 tangu kuanza kwa vita dhidi ya uvamizi wa Japan (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 08, 2024
China yafanya shughuli ya kukumbuka miaka 87 tangu kuanza kwa vita dhidi ya uvamizi wa Japan
Kwaya ya wanafunzi wa chuo kikuu ikiimba kwenye shughuli ya kukumbuka miaka 87 tangu kuanza kwa vita ya China dhidi ya uvamizi wa Japan kwenye Jumba la Makumbusho ya Vita ya Watu wa China dhidi ya Uvamizi wa Japan mjini Beijing, China, Julai 7, 2024. (Xinhua/ Li Xiang)

BEIJING - China imefanya shughuli ya kukumbuka miaka 87 tangu kuanza kwa vita yake ya dhidi ya uvamizi wa Japan siku ya Jumapili ambapo Yin Li, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Katibu wa Kamati ya CPC ya Mji wa Beijing, aliongoza shughuli hiyo kwenye Jumba la Makumbusho ya Vita ya Watu wa China dhidi ya Uvamizi wa Japan karibu na Daraja la Lugou, ambako Tukio la kihistoria la Daraja la Lugou lilitokea miaka 87 iliyopita.

Julai 7, 1937, wanajeshi wa Japan walishambulia vikosi vya China kwenye Daraja la Lugou, ikiashiria mwanzo wa uvamizi kamili wa Japan dhidi ya China, na mapambano ya China nzima dhidi ya wavamizi wa Japan.

Saa tatu asubuhi, shughuli hiyo ilianza kwa kuimba wimbo wa taifa la China. Mashairi yalisomwa na nyimbo ziliimbwa na wanafunzi kutoka mji mkuu huo wa China ili kueleza azma ya kizazi kipya ya kuendeleza moyo wa mashujaa na watu waliojitoa mhanga, kuendeleza ujenzi wa mambo ya kisasa wa China na kutoa mchango kwa ajili ya kujenga taifa lenye nguvu na kutimiza ustawishaji wa taifa la China.

Watu waliohudhuria walitoa maua na kuinama kutoa heshima zao kwa wale ambao walijitoa maisha yao katika mapambano dhidi ya uvamizi wa Japan.

Shughuli hiyo ilihudhuriwa na watu takriban 500, wakiwemo maveterani wa vita na wanafamilia wa maafisa wa kijeshi katika vita hivyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha