

Lugha Nyingine
Mji wa Beijing, China watikiswa kwa midundo ya utamaduni wa kipekee wa Afrika
![]() |
Watu wakitazama kazi za mikono za Afrika kwenye Duka la Sanaa katika eneo la Chaoyang, Beijing. [Picha na Tian He/China Daily] |
Wachina wengi wanaona Afrika ina ardhi yenye mandhari nzuri ya asili na wanyama pori, lakini ufahamu kuhusu utamaduni wake tajiri haujulikani sana.
Mjini Beijing, China wapenzi wa utamaduni na wale ambao wameishi au kutembelea Afrika wanajaribu kuimarisha uhusiano wa kitamaduni na bara hilo kwa kutambulisha sanaa na ufundi wake wa kipekee kwa wakaazi.
Azma yao katika kuitangaza Afrika pia inaongeza msisimko kwa mji mkuu huo wa China kupitia kumbi zinazoruhusu watalii kujionea utamaduni wa Afrika.
Feng Xinxin, ambaye ana umri wa miaka 30, amewahi kuishi Namibia kwa miaka 11 kuanzia Mwaka 2008. Michoro, sanamu na picha zake za wanyama adimu wa Afrika zinaonyeshwa kwenye mkawa wenye mambo ya Kiafrika katika bustani ya kitamaduni nje ya Barabara ya Mzunguko wa tano ya Mji wa Beijing upande wa kaskazini mashariki.
"Niliporudi (kutoka Namibia), na kuzungumza na watu walio karibu yangu, swali lao la kwanza kuhusu Afrika lilikuwa kama ni sehemu yenye vita na kama kwenda huko hakukuwa salama," amesema Feng. "Watu walikuwa wakishangaa kwa nini mwanamke aweze kwenda Afrika katika umri mdogo, na walikuwa na hali ya kushuku.
"Nilikuwa nikiulizwa maswali mengi na hii ikawa motisha kwangu kujenga mahali kama hayo hapa Beijing, ili kuwafanya watu wengi zaidi kuelewa Afrika."
Uhusiano maalum
Mwaka 2022, yeye na mshirika wake walifungua Kituo cha Utamaduni na Utalii wa Afrika, ambacho ni mkahawa wenye sehemu ya kuonyesha bidhaa kutoka Afrika, kwa wazo la kutangaza vyakula, sanaa na utamaduni wa Afrika.
Feng, ambaye ni mzaliwa wa Jinan, Mkoa wa Shandong, amesema alianzisha uhusiano maalum na Namibia, ambao ameuelezea kuwa usio wa kawaida wa nchi za Afrika Magharibi, wakati alipokuwa akiishi Namibia. Amesema nchi hiyo ina jangwa kongwe zaidi duniani, la Namibia ambalo liko karibu na pwani.
Aina mbalimbali za kazi za mikono zilizalishwa kwa chochote kilicho karibu, kama vile vinyago vya mbao, mawe na mayai. Wasanii na mafundi wa kazi za mikono wengi wa Afrika hawajafunzwa rasmi, jambo ambalo linawapa uhuru zaidi wa kuwa wabunifu, amesema.
Moja kwa moja, yenye nguvu
Maoni ya Feng yanaungwa mkono na Tian He, mwongozaji wa filamu anayeishi mjini Beijing ambaye amefungua jumba la kazi za mikono na sanaa za Afrika. Duka la Sanaa la Mwongozaji linajieleza kama jumba la makumbusho ya Afrika mjini Beijing linaloonyesha sanaa, na mila na tamaduni mbalimbali za makabila tofauti ya bara hilo.
"Ufundi wa kazi za mikono wa Afrika unanivutia kwa sababu siyo tu kwamba ni wa kipekee, lakini rahisi, wa moja kwa moja, na wenye nguvu ya ajabu," amesema, akiongeza kuwa sanaa ya Afrika ni moja kwa moja na kama ya kitoto katika usafi wake.
Sanaa yenye uhalisia uleule wa kale
Kazi za mikono zaidi ya 800, zikiuzwa kuanzia yuan 10 hadi 100,000 ($ 1.3 hadi $ 13,757), zimejazwa pomoni kwenye ghorofa ya kwanza ya duka la Tian.
Duka hilo lenye ukubwa wa kati ni kama njia ya kuelekea dunia tofauti, ambayo kwa mujibu wake, linaonyesha uhalisi wa sanaa ya Afrika.
“Lugha barani Afrika kwa kiasi kikubwa zimefanywa kuwa za Kimagharibi, huku Kifaransa na Kiingereza ndizo lugha rasmi katika nchi nyingi barani humo,” amesema Tian.
"Hata hivyo, sanaa za muundo wa kijadi wa Afrika zimeendelea kuwa zilezile hadi leo, zikiwakilisha utambulisho wa kitamaduni wa jamii nyingi na kuwa chanzo cha mapato kwa mafundi wenyeji.
Muziki wa furaha
Muziki wa Afrika, haswa midundo yake maarufu, pia unazidi kupata umaarufu mjini Beijing.
Kwenye kituo cha kujifunza muziki kaskazini mwa Beijing, wanafunzi wenye umri wa kuanzia miaka 7 hadi 50 wanajifunza kucheza ngoma za Afrika na midundo nyumbuliko inayolitambulisha bara hilo.
Mwalimu, Liu Yaoli, mwenye umri wa miaka 27 kutoka Guiyang, Mkoa wa Guizhou, amesema: "Kupitia muziki na ukuzaji ujuzi, wanafunzi wanaweza kupata ufahamu wa mdundo na wakati, kuwaruhusu kuongeza nguvu wakati wanapocheza.
Muunganisho na Afrika
Waafrika pia wanaacha nyayo zao mjini Beijing kupitia maingiliano kati yao na wakaazi.
Davis Murima, afisa biashara mwenye umri wa miaka 32 kutoka Wizara ya Biashara, Uwekezaji na Viwanda ya Kenya, kwa sasa yuko Beijing kwenye programu ya mabadilishano katika Chuo Kikuu cha Biashara na Uchumi wa Kimataifa. Tangu Agosti, amejitolea kwa mlezi katika Kituo cha Utamaduni na Utalii cha Feng, akichangia ujuzi wake na kuwaeleza watalii wake maelezo kuhusu maonyesho hayo.
“Nikiwa hapa, najifunza mengi kuhusu jinsi Wachina wanavyopenda kuelewa utalii, kilimo na utamaduni barani Afrika, na siwezi kuzungumza na Wachina pekee bali watu tofauti kutoka mabara mengine,” amesema Murima.
"Inanipa njia ya kuelewa jinsi utamaduni unavyowafanya watu kuwa tofauti, na anuai ya sehemu mbalimbali."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma