Mji wa Chongqing, China washuhudia ongezeko la watalii wa kigeni kufuatia hatua wezeshi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 10, 2024
Mji wa Chongqing, China washuhudia ongezeko la watalii wa kigeni kufuatia hatua wezeshi
Afisa wa polisi akishughulikia taratibu za kuingia kwa abiria kutoka Australia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chongqing Jiangbei, mjini Chongqing, Kusini-Magharibi mwa China, Julai 2, 2024. (Picha na Zhang Shaobo/Xinhua)

Mji wa Chongqing, Kusini-Magharibi mwa China umehudumia abiria zaidi ya 150,000 wanaoingia na kutoka nje ya China katika nusu ya kwanza ya mwaka huu wa 2024, ikiwa ni mara 4.9 zaidi ya idadi hiyo ya mwaka jana wakati kama hicho mwaka jana.

Kutokana na sera za visa zilizoboreshwa, Chongqing inaendelea kuboresha usimamizi wa taratibu za safari kwa vikundi vya watalii wanaoingia kutoka nje ya China, ikiwapa wasafiri wa kigeni machaguo wezeshi zaidi kwenye bandari za kuingia na kutoka. Wakati huo huo, mfumokazi wa kuratibu visa umeanzishwa kati ya bandari za Mji wa Chongqing na Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha