Mwanasayansi mkuu wa darubini ya FAST ya China atunukiwa Tuzo ya Marcel Grossmann

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 10, 2024
Mwanasayansi mkuu wa darubini ya FAST ya China atunukiwa Tuzo ya Marcel Grossmann
Mnajimu wa redio wa China Li Di (Kulia), ambaye pia ni mwanasayansi mkuu wa Darubini ya Redio ya Uwazi wa Mviringo ya Mita-mia-tano ya China Aperture Spherical Radio Telescope(FAST), akitunukiwa Tuzo la Marcel Grossmann huko Pescara, Italia, Julai 9, 2024. (Xinhua/Li Jing)

PESCARA, ITALIA –Mnajimu wa redio wa China Li Di (Kulia), ambaye pia ni mwanasayansi mkuu wa Darubini ya Redio ya Uwazi wa Mviringo ya Mita-mia-tano ya China Aperture Spherical Radio Telescope(FAST), ametunukiwa tuzo ya Marcel Grossmann siku ya Jumanne kwa mchango wake wa utafiti katika nyanja ya mlipuko wa haraka wa redio (FRBs) akiwa ni mwanasayansi wa kwanza wa China kupokea tuzo hiyo ya kifahari ya fizikia kwa mafanikio yaliyopatikana nchini China.

Li ametunukiwa tuzo hiyo kwa mchango wake mkubwa katika uwezo wa kisayansi wa darubini nyeti zaidi ya redio duniani, ikiwa ni pamoja na vipimo sahihi vya nyanja za sumaku za karibu na nyota na kuendeleza utafiti wa FRBs kufikia umuhimu wa juu wa kitakwimu, kwa mujibu wa kamati ya Mkutano wa 17 wa Marcel Grossmann, ambao unaendelea kwa sasa huko Pescara, Italia, hadi Ijumaa.

"Wanadamu wana anga moja, na ufunguaji mlango wa kimataifa wa unajimu hauepukiki," Li ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano.

"Kuimarisha ushirikiano kati ya China na Umoja wa Ulaya, hasa kupitia ugavi wazi wa data za unajimu kati ya pande hizo mbili, kunaweza kuendeleza uchunguzi wa hali ya juu na kuzuia kwa njia ifaayo kutengana." amesema.

"Michango ya hivi karibuni ya Li, haswa katika nyanja za FRB za ajabu, umesogeza uelewa wetu mbele," amesema Michael Kramer, mkurugenzi wa Taasisi ya Max Planck ya Unajimu wa Redio.

Mchango ongozi wa kisayansi wa Li katika mradi wa darubini ya FAST na uvumbuzi unaowezeshwa na chombo hiki cha ajabu hufanya tuzo hii kuwa ya kipekee, Kramer ameongeza.

Tuzo ya Marcel Grossmann, iliyoanzishwa Mwaka 1985 na hutolewa kila baada ya miaka mitatu, inaelezwa kuwa moja ya tuzo za kimataifa za kifahari zaidi katika fizikia. Washindi wa awali wa China ni pamoja na washindi wa Tuzo ya Nobel Yang Zhenning na Li Zhengdao, pamoja na mwanahisabati wa kiwango cha dunia Qiu Chengtong.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha