Wanafunzi wa kimataifa wafurahia “Kusafiri kutalii China” katika mji wa Chongqing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 15, 2024
Wanafunzi wa kimataifa wafurahia “Kusafiri kutalii China” katika mji wa Chongqing
Ilia Anfilatov (kulia) na Syyra Alee wakipiga video kwenye bustani ya kitamaduni iliyoko Wilaya ya Yuzhong ya Mji wa Chongqing, China, Julai 12, Mwaka 2024. (Mpiga picha:Tang Yi/Xinhua)

Wanafunzi wa kimataifa Ilia Anfilatov anayetoka Russia na Syyra Alee anayetoka Pakistan wamekuwa wakisoma katika Chuo Kikuu cha Kusini Magharibi mjini Chongqing, China kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Katika wakati wao wa mapumziko, hufurahia kufanya matembezi ya kuzunguka mji huo na kuchapisha kwenye mitandao ya kijamii mambo na mandhari nzuri wanazokuwa wanajionea.

Kutokana na machapisho ya maudhui yao mtandaoni, marafiki na jamaa zao wengi huvutiwa na mandhari nzuri na utamaduni anuai wa China na kupanga kufanya safari kuja China na kujionea nchi hiyo wenyewe katika siku za usoni.

Hivi karibuni, “kusafiri kutalii China” imekuwa neno linalotafutwa zaidi kwenye majukwaa mengi ya mitandao ya kijamii duniani wakati ambapo watalii wa kimataifa wanamiminika kwenye maeneo ya vivutio maarufu vya watalii vya China na kuchapisha mtandaoni simulizi za wanakotalii na wanayojionea.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha