Kijana wa Ubelgiji aishi maisha ya kawaida na ya furaha pamoja na wazazi wake kijijini katika mkoa wa Guizhou, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 15, 2024
Kijana wa Ubelgiji aishi maisha ya kawaida na ya furaha pamoja na wazazi wake kijijini katika mkoa wa Guizhou, China
Kevin Cillen Michael E. akichota maji kutoka kwenye kifaa cha kuvuna maji ya mvua katika shamba lake lililoko Kijiji cha Xiasi, Wilaya ya Dushan, Mkoa wa Guizhou, kusini-magharibi mwa China, Juni 13, 2024.(Xinhua/Tao Liang)

Katika Kijiji cha Xiasi, Wilaya ya Dushan, Mkoa wa Guizhou, kusini-magharibi mwa China kuna shamba la kipekee la kiikolojia la familia. Linaendeshwa na Kevin Cillen Michael E., Mbelgiji mwenye umri wa miaka 28 ambaye ana shauku kubwa kwa ardhi hiyo.

Kwa pamoja na wazazi wake na kaka zake, wamechanganya mbinu za kilimo za nchi za Magharibi na zile za kijadi za wenyeji za kijijini ili kukuza "oasisi ya ikolojia" katika eneo la pembezoni milimani.

Ikiwa imezungukwa na vilima vya kijani na milio ya kuvutia ya ndege, familia hiyo imejitoa kwa ajili ya ardhi hiyo, ikiendeleza bila kuchoka ndoto yao ya ukulima nchini China. Safari yao ilianza Mwaka 2000 wakati mama yake Kevin, Hetty Cillen Bottheft, alipotembelea China akiwa ni mfanyakazi wa kujitolea kwa mara ya kwanza. Mandhari ya kuvutia na utamaduni wa Guizhou ilimvutia, na kumhimiza kuifanya nchi hii ya kigeni kuwa maskani yake. Muda mfupi baadaye, baba yake Kevin, Patrick Jan Cillen, alijiunga naye mkoani Guizhou.

Mwaka 2017, familia hiyo ilianza ukurasa mpya, ikihamia Mji mdogo wa Xiasi kukodisha shamba katikati ya msitu wa eneo hilo na kuanzisha shamba la kiikolojia. Kuanzia hatua ya kwanza kabisa, waliweka msingi, kusawazisha ardhi, kupanda malisho, na kununua vitoto vya kondoo na vifaranga kwa ajili ya kufuga.

Baada ya zaidi miongo miwili nchini China, Kevin na familia yake wanaichukulia Guizhou kuwa maskani yao. Wana matumaini kuwa: kujikita katika kilimo cha ikolojia, kutafuta aina mpya za kilimo, na kuhamasisha ufahamu wa mazingira kupitia mitandao ya kijamii ili kuvutia umakini zaidi katika kilimo cha ikolojia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha