Kampuni ya magari ya FAW ya China yashuhudia lori la Jiefang linalofikia No.9,000,000 likiondoka kwenye mstari wa uundaji kiwandani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 17, 2024
Kampuni ya magari ya FAW ya China yashuhudia lori la Jiefang linalofikia No.9,000,000 likiondoka kwenye mstari wa uundaji kiwandani
Gari linalofikia No.60,000,000 yaliyoundwa na Kundi la Kampuni za Magari ya FAW ambalo pia ni gari linalofikia No.9,000,000 yaliyozalishwa na Kampuni ya Magari ya FAW Jiefang likitoka kwenye mstari wa uundaji kiwandani huko Changchun, Mkoa wa Jilin, kaskazini mashariki mwa China, Julai 16, 2024. (Xinhua/Yan Linyun)

CHANGCHUN - FAW Jiefang, kampuni tanzu ya Kundi la Kampuni za Magari za FAW za China, imeshuhudia gari lake linalofikia No.9,000,000 yaliyozalishwa tangu kuanzishwa kwake likitoka kwenye mstari wa uundaji kiwandani siku ya Jumanne, likifanya jumla ya magari yaliyozalishwa na kundi hilo la kampuni kufikia milioi 60.

FAW Jiefang ilizalisha malori 143,300 katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, ikiwa ni ongezeko la asilimia 4.11 kuliko mwaka uliopita  na mauzo yalipanda kwa asilimia 15.4 hadi kufikia malori 151,800 katika kipindi hicho.

Ikiwa imejikita katika kuimarisha teknolojia zake kuu, FAW Jiefang itaendelea kuboresha uvumbuzi na huduma zake, amesema Qiu Xiandong, meneja mkuu wa kampuni hiyo.

Likiwa lilianzishwa Mwaka 1953 na kuwa na makao yake makuu katika Mkoa wa Jilin, kaskazini-mashariki mwa China, Kundi la Kampuni za Magari za FAW linalomilikiwa na serikali ya China linajulikana kama msingi wa sekta ya magari ya China. Lori la kwanza la kampuni hiyo ya Jiefang lilitoka kwenye mstari wa uundaji kiwandani Mwaka 1956. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha