

Lugha Nyingine
Wafanyakazi wa huduma za afya nchini Sudan Kusini wapata mafunzo ya lugha ya Kichina (3)
![]() |
Mu Jianjun (wa tano, kulia, mbele), balozi mdogo wa China anayeshughulikia masuala ya uchumi na biashara nchini Sudan Kusini, akiwa katika picha ya pamoja na Chen Si (wa sita, kulia, mbele), kiongozi wa kundi la 11 la timu ya madaktari wa China nchini humo, na wengine mjini Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, Julai 17, 2024. (Picha na Denis Elamu/Xinhua) |
JUBA - Kozi ya nne ya lugha ya Kichina kwa wahudumu wa afya nchini Sudan Kusini imeanza siku ya Jumatano, ikivutia wanafunzi wapatao 100 wenye shauku ya kujifunza na kutumia fursa zinazotokana na kujifunza lugha ya Kichina.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Isaac Maker, mkurugenzi wa tiba wa Hospitali ya Teaching ya Juba, amehimiza wanafunzi hao kujifunza lugha hiyo ambayo ni moja ya lugha muhimu zaidi duniani.
Maker amesema kuwa umahiri wa lugha ya Kichina utatoa fursa kwa madaktari kuendeleza masomo yao na kupata ujuzi mpya chini ya mpango wa mawasiliano kati ya watu unaotekelezwa hivi sasa na serikali za China na Sudan Kusini.
"Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kazi inayofanywa na madaktari wa China katika hospitali ya Teaching ya Juba. Wanasaidia sana watu wa Sudan Kusini na naishukuru serikali ya China kwa kuleta madaktari hapa na Afrika nzima," Maker amesema huko Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini.
Mu Jianjun, balozi mdogo wa China anayeshughulikia Masuala ya Uchumi na Biashara nchini Sudan Kusini, amesema watu wa Sudan Kusini wamekaribisha kwa furaha lugha ya kichina na utamaduni wa jadi wa China.
Mu amebainisha kuwa kozi hiyo ya lugha ya Kichina inalenga kusaidia wahudumu wa afya wa Hospitali ya Teaching ya Juba kuwasiliana vyema na timu ya madaktari wa China, kuelewa lugha ya Kichina na utamaduni wa China, na kuzidisha urafiki kati ya China na Sudan Kusini.
"Timu ya madaktari wa China imekuwa ikijulikana na kupendwa na watu wengi zaidi nchini Sudan Kusini," amesema.
Chen Si, kiongozi wa kundi la 11 la timu ya madaktari wa China nchini humo, amesema kozi hiyo ya lugha ya Kichina inalenga kuzidisha zaidi maelewano na kuimarisha urafiki kati ya nchi hizo mbili na watu wao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma