Ushirikiano kati ya China na Afrika wasaidia kustawisha kijiji cha Cameroon (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 25, 2024
Ushirikiano kati ya China na Afrika wasaidia kustawisha kijiji cha Cameroon
Watoto wakicheza kwenye Shule ya Chekechea na Msingi ya Ndoumale katika Kijiji cha Ndoumale nje kidogo ya Kribi, Cameroon, Julai 10, 2024. (Picha na Kepseu/Xinhua)

YAoundE - Kijiji cha Ndoumale kusini mwa Cameroon kilikuwa kikiwajia akilini watu kwa karibu kila kitu isipokuwa maendeleo. Kikiwa kinapatikana nje kidogo ya mji wa pwani wa Kribi, kijiji hicho ambacho hapo awali kilikuwa hakifikiki kwa urahisi, sasa kinaongeza ustawi wake kutokana na utekelezaji wa miradi ya ushirikiano kati ya China na Afrika.

Mabadiliko makubwa ya kijiji hicho yalianza Mwaka 2011 wakati kampuni ya uhandisi wa ghuba ya China (CHEC), ilipoanza kujenga awamu ya kwanza ya Bandari ya Kina kirefu ya Kribi umbali wa kilomita takriban 25 kutoka kijijini hapo.

Mtandao wa Barabara na Madaraja

Ili kufika Ndoumale, mtu alilazimika kusafiri kwa angalau saa mbili kupitia njia makorongo na yenye matope.

"Ilikuwa njia ya maji ambayo haikuwa na daraja. Hapakuwa na barabara," amesema Henri Bikouo, kiongozi wa kijiji hicho.

Mambo ni tofauti sasa. Kama sehemu ya wajibu wake wa kijamii, CHEC imejenga barabara na madaraja katika kijiji hicho.

Mtandao wa barabara ulienea hadi eneo la Bagyeli la pygmy, kabila la kiasili.

Shule ya watoto wenye madarasa sita

Katika kijiji hicho cha Ndoumale, watoto walilazimika kusafiri kwa kilomita tisa kutafuta shule ya karibu kwa sababu hakukuwa na shule katika kijiji hicho, amesema Bikouo, ambaye watoto wake sita walikaribia kuacha shule kutokana na hatari na gharama iliyohusika katika safari hiyo ndefu.

Kuna matumaini sasa.

Wakati waandishi habari wa Shirika la Habari la China, Xinhua walipofika katika kijiji hicho, Brian Mengue mwenye umri wa miaka 10 ambaye ana ndoto za kuwa daktari alikuwa na pilika nyingi akihudhuria masomo na marafiki zake katika Shule ya Chekechea na Msingi ya Ndoumale.

Jengo hilo lenye vyumba sita vya kulala lilikuwa likitumiwa na wafanyakazi Wachina wa CGCOC waliokuwa wakijenga mtambo wa maji, lakini waliporudi China baada ya kumaliza mradi huo, jengo hilo liligeuzwa kuwa shule.

Ni shule pekee ya msingi katika kijiji hicho na imekuwa ikifanya kazi kwa miaka mitatu.

Usiku wa giza waangaziwa

Usiku unapoingia katika kijiji hicho cha Ndoumale, taa za umeme unaozalishwa kwa nishati ya jua zinawashwa kuangazia Shule ya Chekechea na Msingi ya Ndoumale, ambayo sasa pia inatumika kama majengo ya shughuli za sherehe na hafla katika kijiji hicho.

Taa hizo zilitolewa na CHEC ili kurahisisha elimu ya watoto na shughuli za usiku kijijini hapo.

"Udahiri wa wanafunzi wa mwaka ujao shuleni hakika utaongezeka kutokana na mwanga huo," amesema Edjenguele, mkuu wa shule hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha