Mji wa Zixing wahamisha wakaazi kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi katika Mkoa wa Hunan, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 31, 2024
Mji wa Zixing wahamisha wakaazi kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi katika Mkoa wa Hunan, China
Picha ya droni iliyopigwa tarehe 30 Julai 2024 ikionyesha mandhari ya tarafa ya Kabila la Wayao ya Bamianshan, Mji wa Zixing, Mkoa wa Hunan katikati ya China. (Xinhua/Chen Zhenhai)

Katika mji wa Zixing wa Mkoa wa Hunan, katikati ya China mvua kubwa iliyosababishwa na kimbunga Gaemi imesomba au kuharibu nyumba za kaya 867 na kusababisha makorongo 1,345 ndani ya barabara. Maofisa wa serikali katika mji huo wamesema kuwa mawasiliano ya simu katika vijiji vingi yalikuwa yametatizwa, ikisumbua habari mpya kupatikana kwa wakati kuhusu hali halisi ya maafa.

Waokoaji zaidi ya 5,400 wametumwa. Jumla ya watu 11,379 wamehamishwa kwa usalama, yamesema idara ya udhibiti wa mafuriko na kupambana na ukame ya mji huo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha