Reli mpya ya mwendo kasi yazinduliwa ili kuimarisha maendeleo jumuishi ya Delta ya Mto Yangtze wa China (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 31, 2024
Reli mpya ya mwendo kasi yazinduliwa ili kuimarisha maendeleo jumuishi ya Delta ya Mto Yangtze wa China
Dreva wa treni ya mwendokasi akifanya kazi ndani ya treni ya majaribio ya mwendokasi ya G55701 kwenye reli mpya ya mwendokasi inayounganisha Hangzhou na Wenzhou huko Jinhua, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Julai 30, 2024. (Xinhua/Jiang Han)

HANGZHOU - Reli mpya ya mwendo kasi yenye urefu wa kilomita 260 na kusanifiwa kuwa na kasi ya kilomita 350 kwa saa imeanza kufanya kazi kwa majaribio siku ya Jumanne ikiunganisha miji miwili muhimu na yenye uchumi mkubwa ya Hangzhou na Wenzhou katika eneo la Delta ya Mto Yangtze, mashariki mwa China.

Reli hiyo ina stesheni tisa, zinazotoa suluhu ya haraka ya usafiri kando ya njia inayounganisha miji muhimu ya kiuchumi ya Hangzhou, Yiwu na Wenzhou katika eneo la delta hiyo linalojulikana kama mojawapo ya maeneo yenye uchumi uliostawi na mkubwa zaidi nchini China.

Wang Chang, msimamizi wa mradi huo wa reli anayefanya kazi kwenye kampuni tanzu ya reli ya Taasisi ya Maendeleo na Mipango ya Mkoa wa Zhejiang, amesema mradi huo wa reli ni majaribio ya kitaifa ya mageuzi ya umiliki mchanganyiko kwa kuvutia mtaji wa kijamii katika ujenzi wa reli.

Reli hiyo ya kati ya miji imeunganishwa na mtandao wa reli ya mwendo kasi katika eneo hilo la delta. Rasilimali tajiri za utalii ikiwa ni pamoja na Hangzhou, na vilevile Mlima Xianhua na Mto Nanxi zimeunganishwa kwenye njia hiyo.

Njia hiyo ya reli ina umuhimu mkubwa katika kuwezesha usafiri wa umma na kukuza maendeleo jumuishi yenye ubora wa juu ya Delta ya Mto Yangtze, amesema Wang.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha