

Lugha Nyingine
Katika picha: Michoro ya mkulima wa Sanjiang katika Mkoa wa Guangxi, China
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 01, 2024
Ikiwa na historia ya miaka mingi, michoro ya mkulima wa Sanjiang katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China inaangazia mila na desturi za watu wa kabila la Wadong. Ikiwa ni urithi wa kitamaduni usioshikika wa mkoa huo, michoro ya mkulima wa Sanjiang inaonesha maisha halisi ya vijijini kwa mitindo ya kipekee ya kikabila.
Wasanii wakulima hunakshi maisha katika uzuri wa vijijini kupitia sanaa zao, na hii, kwa upande mwingine, huwasaidia katika kuongeza mapato yao. Wasanii-wakulima zaidi ya 600 wanajishughulisha na tasnia ya uchoraji katika wilaya hiyo, ikiwapatia mapato ya yuan zaidi ya milioni 5 (dola za Kimarekani kama 692,570) kila mwaka.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma