Injini ya kutumia umeme inayojiendesha yenyewe bila dereva yakamilika kuundwa huko Xi’an, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 05, 2024
Injini ya kutumia umeme inayojiendesha yenyewe bila dereva yakamilika kuundwa huko Xi’an, China
Injini ya kutumia umeme inayojiendesha yenyewe bila dereva ambayo imesanifiwa na kuundwa kwa kujitegemea na Kampuni ya Chang’an Zhonggong ya Kundi la Kampuni za Reli la China (REC) imekamilika kuundwa Agosti 1 katika Eneola Yanliang, mji wa Xi’an, China.

Inafahamika kuwa, chombo hicho hutumika zaidi katika mazingira ya kazi ya ndani ya handaki, kikiwa kimefungwa vifaa vya kamera zenye kupiga picha za ubora wa juu, lada ya kukusanya data kwa usahihi wa juu zaidi na vifaa vingine. Kina uwezo wa ukwepaji kiotomatiki wa vizuizi na kujitambua hitilafu zake chenyewe na uwezo mwingine, kikiweza kuonesha data husika na kujiendesha bila ya dereva katika mchakato mzima wa “kupakia, kuhamisha na kupakua”.

Picha na Zhang Bowen/Xinhua

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha