

Lugha Nyingine
China yashinda medali ya dhahabu kwa mbio za kuogelea kwa kupokezana wachezaji wanne za Mita 100 kwa wanaume katika Michezo ya Olimpiki ya Paris (2)
China imeshinda medali ya pili ya dhahabu katika mchezo wa mbio za kuogelea kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris siku ya Jumapili, kwa kushinda fainali ya mbio za kuogelea kwa kupokezana wachezaji wanne za Mita 100 kwa wanaume.
Timu ya wachezaji wanne wa China ambao ni Xu Jiayu, Qin Haiyang, Sun Jiajun na Pan Zhanle iligusa ukuta kwa kuogelea kwa muda wa dakika 3 na sekunde 27.46, zaidi ya nusu sekunde mbele ya Timu ya Marekani yenye kujumuisha Ryan Murphy, Nick Funk, Kaleb Dressel na Hunter Armstrong, ambayo ilitumia dakika 3 na sekunde 28.01.
Timu ya Ufaransa inayojumuisha John Ndoye-Brouard, Léon Marchand, Maxime Grusset na Florent Manadoux imeshinda medali ya shaba kwa kuogelea kwa muda wa dakika 3 sekunde 28.38.
Mafanikio hayo yamevunja rekodi ya Marekani ya kuchukua medali 10 za dhahabu mfululizo katika mchezo huo tangu Michezo ya Olimpiki ya Los Angeles ya Mwaka 1984.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma