Lugha Nyingine
Zou Jingyuan ashinda medali ya pili ya dhahabu ya China ya mchezo wa Jimnastiki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris
PARIS - Zou Jingyuan alijitahidi kushinda jeraha la bega na kutwaa taji la jimnastiki za kisanii kwenye milingoti sambamba kwa wachezaji wa kiume siku ya Jumatatu na kuipatia China medali ya pili ya dhahabu ya jimnastiki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris ambapo bingwa huyo mtetezi Zou ni mchezaji pekee wa tatu duniani kushinda medali mbili za dhahabu mfululizo kwenye mashindano ya mchezo huo, akikusanya pointi nyingi 16.200 kumshinda Illia Kovtun wa Ukraine, ambaye alichukua medali ya fedha kwa kupata pointi 15.500.
Shinnosuke Oka wa Japan, bingwa wa jimnastiki ya pande zote, amepata medali ya shaba kwa kujipatia pointi 15.300.
Zou alionekana akiuguza bega lake la kulia baada ya fainali ya jimnastiki ya kujiviringisha na kunyumbua viungo kwa kushikilia pete zenye kuning’inia kwenye kamba mbili siku ya Jumapili, ambapo aliweza kupata medali ya fedha. Alisema baadaye jeraha hilo liliathiri mazoezi yake.
Minyumbuliko ya Zou yenye kukaribia ukamilifu ilivuta hisia kutoka kwa umati kwenye kiwanja cha mashindano cha Bercy. Alikuwa katika udhibiti kamili na kuruka juu ya milingoti kwa miunganisho laini.
Mwenzake Zhang Boheng ambaye ndiyo kwanza ameshinda medali ya fedha ya jimnastiki ya pande zote kwa wanaume amemaliza wa nne katika shindano hilo la Jumatatu.
Mali ya Urithi wa Utamaduni Usioshikika Kando Mbili za Mfereji Mkuu wa China Yaonyeshwa Mkoani Hebei
Michezo ya Kupanda Farasi ya"Agosti Mosi" yaanza katika Wilaya ya Litang Mkoa wa Sichuan, China
Mashindano ya kimataifa ya boti za matanga yamalizika huko Dalian, China
Watalii watembelea eneo lenye mandhari nzuri la Mlima Fairy la Chongqing, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma