

Lugha Nyingine
Xinjiang yaanzisha mradi wa kupeleka maji kwenye mto mrefu zaidi wa maeneo ndani ya China (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 13, 2024
Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China siku ya Jumatatu umeanza kupeleka maji kutoka kwenye Bwawa hadi kwenye Mto Tarim, ambao ni mto mrefu zaidi wa ndani ya China, ikiwa ni sehemu ya mradi wa uhifadhi wa ikolojia unaoendelea katika mkoa huo.
Malango katika Bwawa la Daxihaizi yamefunguliwa, yakipeleka maji kwenye Mto Tarim, hii ni raundi ya pili ya mara ya 25 ya kupeleka maji tangu mradi huo uanze Mwaka 2000.
Mkoa huo wa Xinjiang umepanga kupeleka maji ya mita za ujazo milioni 510 mwaka huu ili kujaza maji ya mto kwenye maeneo ya mtiririko wa Mto Tarim na kukidhi usambazaji maji kwa misitu ya populus euphratica, huku mita za ujazo milioni 346 za maji zikiwa zimekamilika ilipofikia Agosti 8.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma