

Lugha Nyingine
Mwanamuziki wa Afrika aeneza muziki katika Mkoa wa Hainan Kusini mwa China
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 16, 2024
![]() |
Picha hii ya kumbukumbu ikionyesha David Mouk (Kulia) akifanya maonyesho kwenye tamasha la muziki huko Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Novemba 2019. (Xinhua/Zhang Liyun) |
Akiwa ni mwalimu wa piano na mwanamuziki wa bendi, David anatoka Jamhuri ya Kongo na amekuwa akiishi katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China kwa miaka karibu 10. Akiwa alisomea muziki tangu utotoni, alianzisha bendi yake akiwa chuoni na baadaye akaja hapa kwa ajili ya kupata shahada ya uzamili.
Mwanamuziki huyo anaamini kabisa kuwa muziki ni sehemu isiyoweza kukosekana ya maisha na inaweza kuleta nguvu kwa watu. Kwa hivyo ameanzisha studio ya muziki kufundisha watoto kupiga piano. Nje ya studio, David hupiga kinanda kwenye bendi mbalimbali.
"Ninaichukulia Hainan kama maskani yangu ya pili na ninatamani kufanya muziki mzuri zaidi hapa," David amesema.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma