China kupanda mpunga kwenye eneo linalotitia kutoka na uchimbaji wa makaa ya mawe

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 28, 2024
China kupanda mpunga kwenye eneo linalotitia kutoka na uchimbaji wa makaa ya mawe
(Picha inatoka VCG)

Baadhi ya mpunga unaolimwa kwa majaribio katika eneo linalotitia kutokana na uchimbaji wa makaa ya mawe umevunwa kwa mara ya kwanza.

Mradi huo kwenye eneo la kutitia kutokana na uchimbaji wa makaa ya mawe kwa lengo la kutimiza “kupanda mpunga juu ya maji na kufuga samaki chini ya maji” ulikamilishwa kwa ushirikiano kati ya Kampuni ya Nishati ya Huaihe na Chuo Kikuu cha Sayansi na uhandisi cha Anhui, ukiwa kwenye mji mdogo wa Guqiao wa Wilaya ya Fengtai ya Mji wa Huainan, Mkoa wa Anhui wa China, na kuhusisha mashamba ya mu 50 (takriban hekta 3.3) ya majaribio ya kupanda mpunga.

Mavuno ya kwanza ya mpunga huo yalikamilika. Timu ya wataalamu walitoa maoni yao ya kutathimini mradi huo kuwa, sifa ya mpunga uliovunwa umefikia kiwango cha kitaifa, na upandaji wa mpunga unasaidia kuboresha ubora wa maji wa eneo husika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha