Ustadi Wenye Historia ya Miaka Elfu Moja Wawezesha Wakulima wa Xizang Kuongeza Mapato

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 03, 2024
Ustadi Wenye Historia ya Miaka Elfu Moja Wawezesha Wakulima wa Xizang Kuongeza Mapato
Wafanyakazi wa Ushirika wa Kitaalamu wa Wakulima wa Bidhaa za Sufu ya rangi ya kahawia ya Yade wakijiandaa kukata vitambaa katika Bustani ya Viwanda Wilayani Renbu, Mjini Shigatse, Mkoa wa Xizang, Septemba 1.(Xinhua/Sun Ruibo)

Ustadi wa kufuma sufu ya rangi ya kahawia ya Yade ni ufundi wa kikabila ambao umeurithishwa kwa miaka karibu elfu moja katika maeneo ya kabila la Watibet. Kitambaa hicho kinatengenezwa kwa michakato kadhaa baada ya kuchagua sufu ya kondoo wa uwanda wa juu ambacho kikiwa laini na kuonyesha uzuri wa utamaduni wa kikabila wa kazi za mkono katika uwanda wa juu. Siku hizi, ustadi huo umehifadhiwa vyema na kurithishwa kupitia njia ya ushirika wa kitaalamu wa ushirikiano wa wakulima na wafugaji katika mji mdogo wa Kangxiong, Wilayani Renbu, Mjini Shigatse, Mkoani Xizang.

Ushirika wa Kitaalamu wa Wakulima wa bidhaa za sufu ya rangi ya kahawia ya Yade katika mji mdogo huo unahamasisha watu wa vijiji vya karibuni kushiriki. Thamani ya uzalishaji ilifikia yuani milioni 20 mwaka 2023 na kuwezesha wakulima kuongeza mapato yao.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha