Lugha Nyingine
Mashindano ya Kimataifa ya Pombe Kali ya Brussels 2024 (Guizhou·Renhuai) yafunguliwa (4)
Mashindano ya Kimataifa ya Pombe Kali ya Brussels 2024 (Guizhou·Renhuai) yamefunguliwa rasmi siku ya Jumanne, Septemba 3 katika Mkoa wa Guizhou, China ambapo katika kipindi cha siku 3 za mashindano hayo, majaji 155 wa kimataifa kutoka nchi na maeneo 40 wataonja wakiwa wamefichwa chapa husika ladha za sampuli za aina 2,811 za pombe kali, na hatimaye kutoa tuzo kwa tuzo kuu tatu za Dhahabu Kubwa, Dhahabu, na Fedha.
Inafahamika kuwa Mashindano ya Kimataifa ya Pombe Kali ya Brussels ni moja ya mashindano matatu makubwa ya pombe duniani, na yanabeba hadhi ya kuwa "Michezo ya Olimpiki ya Pombe Kali." Ikilinganishwa na mashindano yaliyopita, idadi ya sampuli za pombe kali katika mashindano ya mwaka huu imefikia kiwango cha juu zaidi katika historia.
Mji wa Zunyi katika mkoa huo wa Guizhou ni eneo kuu duniani la uzalishaji wa pombe kali aina ya "baijiu" yenye ladha ya soya, na pia ni kituo muhimu cha uzalishaji wa baijiu nchini China.
Katika mashindano hayo, majaji 60 wa kigeni kutoka nchi na maeneo 28 wamechaguliwa kuwa "Mabalozi wa Kimataifa wa Uenezaji wa Zunyi Baijiu yenye harufu ya soya."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma