Lugha Nyingine
Matufaha yaleta Utajiri katika Mji wa Mengzi, Mkoa wa Yunnan, China
Wakulima wakiwa wamebeba matufaha katika Kijiji cha Xibeile, Mji wa Mengzi wa Honghe, Mkoa wa Yunnan, China, Septemba 3. (Xinhua/Hu Chao) |
Hivi karibuni, matufaha katika Kijiji cha Xibeile, Mji wa Mengzi wa Honghe, Mkoa wa Yunnan, China yameingia msimu wa kuiva, na wakulima wako katika pilika za kuyachuma, kuyapanga na kuyasafirisha ili kuyasambaza sokoni.
Kijiji cha Xibeile kiasili ni chenye ardhi ya karst. Kwa sababu ya milima mirefu na miteremko mikali, uoto mdogo wa mimea na mkusanyiko mkubwa wa changarawe, kijiji hicho kilikuwa mlima usioweza kuzalisha mazao ya aina yoyote. Katika miaka ya hivi karibuni, eneo hilo limekuwa likiendeleza kwa uendelevu urejesho wa ikolojia na maendeleo ya uchumi, na kuhimiza kwa nguvu upandaji wa matufaha. Eneo la upandaji matufaha limefikia ukubwa wa mu 52,000 (takriban hekta 3466.67), na mavuno ya kila mwaka yanatarajiwa kuzidi tani 15,000, yakiwezesha wakulima 1,412 wanaopanda matufaha kuongeza mapato yao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma