Rais Xi akaribisha viongozi wa Afrika, asifu uhusiano wa mfano kati ya China na Afrika kabla ya mkutano mkubwa wa kilele wa FOCAC (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 05, 2024
Rais Xi akaribisha viongozi wa Afrika, asifu uhusiano wa mfano kati ya China na Afrika kabla ya mkutano mkubwa wa kilele wa FOCAC
Rais Xi Jinping wa China na mkewe Peng Liyuan, pamoja na wageni wa kimataifa wanaohudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya dhifa ya kukaribisha wageni iliyofanyika kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Septemba 4, 2024. (Xinhua/Ding Lin)

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China amepongeza "mfano bora" wa uhusiano kati ya China na Afrika wakati China ikitandaza zulia jekundu kwa viongozi wa Afrika na wageni wengine walioko Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), hii ni shughuli kubwa zaidi ya kidiplomasia inayoandaliwa na China katika miaka mingi iliyopita, ambapo Xi na mkewe, Peng Liyuan, wamefanya dhifa ya kukaribisha wageni hao kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing.

Mkutano huo unaohudhuriwa na viongozi zaidi ya 50 wa Afrika na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, umeanza rasmi jana Jumatano Septemba 4 na utaendelea hadi kesho Ijumaa Septemba 6.

Akihutubia kwenye dhifa hiyo, Rais Xi amesema, amefanya ziara barani Afrika mara 10, na kwamba jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja ni mfano bora kwa ajili ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Rais Xi amesema jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja imekita mizizi katika urafiki wa jadi kati ya pande hizo mbili, na urafiki huo unaendelea kuwa wa kithabiti na unazidi kuimarika kupitia vizazi vyote bila kujali jinsi dunia inavyobadilika.

"Tumejenga barabara, reli, shule, hospitali, maeneo ya viwanda na maeneo maalumu ya uchumi. Miradi hii imebadilisha maisha na mustakabali wa watu wengi," Rais Xi amesema, akidhihirisha kuwa jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja inastawi kwenye nguvu ya ushirikiano wa kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja.

Rais Xi amesema, jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja inakua sambamba na nyakati, pande hizo mbili zimedumisha ushirikiano na uratibu wa karibu katika masuala makubwa ya kimataifa na kikanda, na kwa pamoja zimeifanya sauti ya nchi za Kusini kuwa na nguvu zaidi.

Kwa upande wake Rais Bassirou Diomaye Faye wa Senegal, ambaye ni mwenyekiti mwenza wa FOCAC, akiwa kwa niaba ya viongozi wa Afrika ametoa shukrani kwa ukarimu wa watu wa China. Amesema, Afrika na China zote zinatetea kujenga dunia iliyo na usawa zaidi, yenye utaratibu, yenye kunufaishana na iliyo jumuishi zaidi.

Faye amesema, chini ya uongozi wa Rais Xi, si tu kwamba China imejipatia maendeleo yake ya haraka bali pia imetoa mchango muhimu kwa ajili ya kuhimiza amani ya dunia na ukuaji wa uchumi wa dunia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha