Lugha Nyingine
China yafanya Maonyesho ya Kimataifa ili kuongeza uwekezaji na biashara
XIAMEN - Maonyesho ya 24 ya Kimataifa ya Uwekezaji na Biashara ya China (CIFIT) yamefunguliwa jana siku ya Jumapili katika mji wa Xiamen, Mkoa wa Fujian wa China, ambapo yakichukua eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 120,000, maonyesho hayo yatakayofanyika kwa siku nne yamevutia washiriki kutoka nchi na maeneo 119, na asilimia 80 kati yao ni washirika wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI).
Maonyesho hayo ya mwaka huu yanaweka mkazo katika kuonesha uchumi wa kidijitali, nishati mpya na uvumbuzi wa kijani. Yanatarajiwa kutumika kama jukwaa la shughuli zaidi ya 80 za uwekezaji na shughuli za maonyesho ya barabarani.
Maonyesho hayo, yanayoandaliwa na Wizara ya Biashara ya China, yalianzishwa mwaka 1997, yamekuwa jukwaa muhimu la kukuza uwekezaji na kuwezesha maendeleo ya kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma