Lugha Nyingine
Vitu vya Utamaduni Usioshikika vyaendelea kurithiwa kando ya Mfereji Mkuu huko Wuxi, Mkoa wa Jiangsu, China
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 11, 2024
Mrithi wa utamaduni usioshikika wa kitaifa wa nakshi kwenye mianzi ya Liuqing ya Wuxi, Qiao Jinhong akiweka nakshi kwenye mianzi, Septemba 10. (Xinhua/Yang Lei) |
Baadhi ya vitu vya urithi wa utamaduni usioshikika kama vile sanamu za udongo za Wuxi, ustadi wa utarizi wa mtindo wa Wuxi na nakshi kwenye mianzi ya Liuqing vilionyeshwa, kufundishwa, kuzalishwa na kuuzwa katika Kijiji cha kale cha Huishan, Mjini Wuxi, Mkoani Jiangsu na kuwezesha watu wengi zaidi kupata uzoefu wa vitu hivi vya urithi wa utamaduni usioshikika kwa karibu.
Tangu 2023, mpango kazi wa miaka mitatu wa Mradi wa Uvumbuzi wa vitu vya Urithi wa Utamaduni Usioshikika wa "Mamia ya Wasanii na Maelfu ya Kazi zao" umezinduliwa katika mji wa Wuxi ili kuboresha kiwango cha kurithi, kuhifadhi na maendeleo ya vitu vya urithi wa utamaduni usioshikika.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma