Chombo cha "Jiaolong" chamaliza kazi ya mwisho ya kuzamia chini baharini katika safari ya kisayansi ya kimataifa kwenye Bahari ya Pasifiki ya Magharibi 2024

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 12, 2024
Chombo cha
Mwanasayansi wa timu ya utafiti Zhang Shan akifanya uchunguzi kwa sampuli ya viumbe iliyochukuliwa wakati wa kuzamia chini baharini tarehe 11, Septemba. (Xinhua/Wang Yuhao)

Saa 7:51 ya tarehe 11 kwa saa za chombo cha “Jiaolong”, chombo hicho kilikamilisha kazi yake ya chini ya bahari ya saa tano na nusu kwenye mlima wa baharini wa Viga katika Bahari ya Pasifiki ya Magharibi, ikibeba waendeshaji wa chombo Zhao Shengya, Zhang Yi, pamoja na mwanasayansi wa timu ya utafiti Gao Wei, na kupanda juu kutoka kwenye sehemu yenye kina cha mita 1,783. Saa 9:10 mchana kwa saa za chombo, "Jiaolong" ilirejea kwenye sitaha ya nyuma ya meli kuu ya "Shenhai-1," hali ambayo inamaanisha kazi yake ya kuzamia chini baharini kwa mara 18 katika safari hiyo ya kisayansi imekamilika kwa mafanikio.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha