Mji wa Mkoa wa Xinjiang waharakisha maendeleo na ujenzi wa vifaa vya nishati ya upepo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 13, 2024
Mji wa Mkoa wa Xinjiang waharakisha maendeleo na ujenzi wa vifaa vya nishati ya upepo
Picha iliyopigwa Septemba 11, 2024 ikionesha mitambo ya kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo na miundombinu ya kuzalisha umeme kwa nishati ya jua kwenye mji mdogo wa Naomaohu wa Mji wa Hami, Mkoa unaojiendesha wa kabila la Wauygur wa Xinjiang nchini China. (Xinhua/Hu Huhu)

Ikiwa na rasilimali nyingi za nishati ya upepo, Hami ni moja kati ya maeneo muhimu ya uzalishaji wa umeme kwa nishati ya upepo nchini China. Ikitumia vizuri rasilimali zake hizo, mji wa Hami umeharakisha maendeleo na ujenzi wa vifaa vya nishati ya upepo katika miaka ya hivi karibuni ili kuhimiza kubadilisha muundo wa nishati kuwa kijani. Wakati huohuo, idadi kubwa ya kampuni za nishati ya upepo nchini China zimeanza kuingia eneo hilo kujenga minyororo ya viwanda ya uundaji wa vifaa vya nishati ya upepo ili kuhimiza maendeleo ya uchumi yenye sifa bora.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha