Lugha Nyingine
Mrithi wa Wimbo wa Kabila la Wadong (6)
Agosti 28, Wu Chunyue(mstari wa kwanza, wa nne kutoka kushoto) na wenyeji wakiimba Wimbo wa Kabila la Wadong kwa kushukuru watalii walioshiriki kwenye karamu katika Kijiji cha Chengyangbacun cha Wilaya inayojiendesha ya Kabila la Wadong ya Sanjiang Mkoani Guangxi, China. (Xinhua/Zhang Ailin) |
Wilaya ya Kabila la Wadong ya Sanjiang ya Mkoa wa Guangxi ambayo ina wakazi wengi zaidi wa Kabila la Wadong nchini China, inajulikana kwa utamaduni wa aina mbalimbali wa Kabila la Wadong. Wimbo wa Kabila la Wadong imeorodheshwa kwenye orodha ya vitu vya urithi wa utamaduni usioshikika wa kitaifa wa China mwaka 2009.
Wu Chunyue mwenye umri wa miaka 37 ndiye mrithi wa Wimbo wa Kabila la Wadong, amejitolea katika uvumbuzi wa kwaya za Kabila la Wadong, akichanganya ala za kijadi na vipengee vya muziki vya kisasa ili kuvumbua mtindo mpya wa kuonyesha. Zaidi ya hayo, Wu Chunyue amekuwa akiendelea kufanya kazi za shambani, kuwasiliana na wanavijiji na watalii wa eneo hilo ili kupata wazo kutoka maisha. Juhudi zake zimevutia vijana wengi zaidi kufuatilia utamaduni wa Kabila la Wadong.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma