Lugha Nyingine
Waandishi wa habari wa nchi za Latin Amerika wajaribu utengenezaji batiki za buluu wa mbinu ya kale katika Kijiji cha Mingyue, mkoani Chengdu, China (3)
Ujumbe wa waandishi wa habari kutoka nchi za Latin Amerika, unaojumuisha waandishi wa habari kutoka Argentina, Brazil, Colombia, Peru na nchi nyingine, walikwenda katika Kijiji cha Mingyue kilichoko Wilaya ya Pujiang, Mji wa Chengdu, Mkoa wa Sichuan, China Septemba 23, ili kujionea mradi wa urithi wa utamaduni usioshikika wa mbinu ya kale ya utengenezaji batiki za buluu na kuhisi hamasa ya urithi wa kitamaduni wa eneo hilo.
Kwa mujibu wa habari zilizotolewa, rangi zilizotumika katika mbinu hiyo ya kale ya utengenezaji batiki za buluu, ni rangi asilia kabisa za mimea zilizotolewa kutoka mmea wa isatis indigotica. Ufundi huu wa kutengeneza batiki ulianzia Enzi za Qin na Han za China ya kale na una historia ya maelfu ya miaka.
Chini ya mwongozo wa mafundi wenyeji, waandishi hao wa habari walishiriki katika mchakato mzima wa utengenezaji batiki na kutengeneza kwa mafanikio kazi za kipekee zenye umaalum wao wenyewe. Pia walielezea kwa hamasa kubwa ufundi huo wa utengenezaji batiki kutoka China kwa hadhira zao. .
Katika miaka ya hivi karibuni, Kijiji hicho cha Mingyue kimekuwa kikitilia maanani utumiaji wa urithi wa utamaduni usioshikika katika kutekeleza kwa vitendo ustawishaji wa vijijini. Kwa kuanzisha chapa maalum za kitamaduni, kimevutia ufuatiliaji kutoka ulimwengu wa nje na kuwa mfano mzuri wa kuigwa wa ustawishaji wa vijijini na maendeleo ya vijijini.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma