Chombo cha China cha Jiaolong cha kuzamia baharini kwa kuendeshwa na binadamu chawasili Hong Kong kwa mara ya kwanza (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 25, 2024
Chombo cha China cha Jiaolong cha kuzamia baharini kwa kuendeshwa na binadamu chawasili Hong Kong kwa mara ya kwanza
Watu wakitembelea maabara ya ikolojia ndani ya meli ya No. 1 ya utafiti wa Bahari ya Kina Kirefu huko Hong Kong, kusini mwa China, Septemba 24, 2024. (Xinhua/Chen Duo)

HONG KONG - Meli ya No.1 ya utafiti wa kisayansi wa Bahari ya Kina Kirefu Baharini ya China ikiwa imebeba chombo cha Jiaolong cha kuzamia baharini kwa kuendeshwa na binadamu, imepata makaribisho mazuri siku ya Jumanne katika Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR), hii ni mara ya kwanza kwa watafiti na vyombo hivyo kutembelea mkoa huo wa China.

Meli hiyo iko katika safari ya kurudi nyumbani baada ya kukamilisha kazi ya kisayansi katika Bahari ya Pasifiki Magharibi. Wakati wa kuwepo kwake kwa siku mbili kwa vyombo hivyo mkoani Hong Kong, wanasayansi walioko ndani yake watatoa mihadhara kwa wanafunzi wa Hong Kong na kufanya makongamano kadhaa ya kimataifa kutoa kwa umma matokeo ya safari yao hiyo ya utafiti wa kisayansi baharini.

Warner Cheuk, naibu ofisa mkuu wa utawala wa serikali ya Hong Kong, amesema kuwa ziara hiyo ya vyombo vya utafiti baharini inayofanyika kabla ya kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China imeonesha serikali kuu inafuatilia na kuunga mkono maendeleo ya utafiti wa kisayansi wa baharini na uhifadhi wa mazingira wa Hong Kong.

Inatarajiwa kwamba shughuli hii itawatia moyo vijana wengi zaidi wa Hong Kong kushiriki katika utafiti wa bahari ya kina kirefu na kuijenga Dunia kuwa mahali pazuri pa kuishi, amesema.

Wu Changbin, mkurugenzi wa Jumuiya ya Utafiti na Uendelezaji wa Rasilimali Madini za Baharini ya China, amepongeza mafanikio ya safari hiyo ya utafiti wa kisayansi wa Bahari ya Pasifiki Magharibi, akisema kwamba safari hiyo si tu imeongeza utambuzi wa kisayansi wa China juu ya bioanuwai na mifumo ya ikolojia ya bahari kuu, lakini pia imechangia data muhimu za kisayansi kwa utafiti wa kisayansi wa baharini wa Dunia.

Timu hiyo ya kundi la watafiti wa kisayansi baharini wa China na wa kigeni ilianza safari yake baharini Agosti 10 kutoka Qingdao, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, na kufanya uzamiaji chini baharini kwa mara 18 katika Bahari ya Pasifiki Magharibi. Na hii ni mara ya kwanza kwa wanasayansi wa kigeni kufanya utafiti wa kisayansi wa bahari ya kina kirefu wakibebwa kwenye chombo cha Jiaolong.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha