Roketi ya Teknolojia za Kisasa ya Dragon-3 ya China yarusha satalaiti 8 kutoka baharini kwenda anga ya juu (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 25, 2024
Roketi ya Teknolojia za Kisasa ya Dragon-3 ya China yarusha satalaiti 8 kutoka baharini kwenda anga ya juu
Roketi ya teknolojia za kisasa ya Dragon-3 ya kubebea satalaiti kwenda anga ya juu iliyobeba satalaiti nane ikiruka kutoka baharini karibu na mji wa Haiyang katika Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, Septemba 24, 2024. (Picha na Guo Houze/Xinhua)

HAIYANG, Shandong - China imerusha roketi ya teknolojia za kisasa ya Dragon-3 ya kubeba satalaiti kwenda anga ya juu kutoka baharini karibu na mji wa Haiyang katika Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China siku ya Jumanne, ikituma satalaiti nane kwenye obiti iliyopangwa ambapo roketi hiyo ya kibiashara iliruka majira ya 4:31 asubuhi (kwa saa za Beijing), ikiwa imebeba Tianyi-41 na satalaiti nyingine.

Kituo cha Urushaji Satalaiti cha Taiyuan kimetekeleza urushaji huo kutoka baharini.

Roketi hiyo ya kubeba satalaiti ya kibiashara ya teknolojia za kisasa ya Dragon-3 imeundwa na Akademia ya China ya Teknolojia za Vyombo vya Kurusha Satalaiti chini ya Shirika la Sayansi na Teknolojia ya Anga ya Juu la China.

Roketi hiyo ya ngazi nne yenye injini thabiti ni aina ya chombo cha kurushwa anga ya juu kwa gharama nafuu na kwa uhakika sana ambacho hutumiwa hasa kurusha vyombo kwenda anga ya juu kwenye obiti sawazishi ya jua au obiti ya chini ya Dunia, limesema shirika hilo.

Aidha, roketi hiyo ina uwezo mkubwa wa kubeba na ni mwafaka kwa kazi mbalimbali za urushaji vyombo kwenda anga ya juu.

Ikiwa na urefu wa mita 31 na kipenyo cha juu cha mita 2.64, roketi hiyo ina uwezo wa kubeba tani takriban 1.5 kwa ajili ya obiti sawazishi ya jua ya kilomita 500, shirika hilo muundaji limesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha