Lugha Nyingine
Watembeleaji wa kimataifa waonja "utamu" wa maonyesho ya aiskrimu ya China (6)
Watu wakitembelea Maonyesho ya Aiskrimu ya China 2024 katika Mji wa Tianjin, kaskazini mwa China, Septemba 26, 2024. (Xinhua/Sun Fanyue) |
TIANJIN - Maonyesho ya Aiskrimu ya China 2024 yameanza siku ya Alhamisi katika Mji wa Tianjin, kaskazini mwa China, yakionyesha bidhaa na teknolojia mpya katika sekta ya aiskrimu. Maonyesho hayo ya siku tatu yamevutia kampuni zaidi ya 450 za ndani na nje ya China na wafanyabiashara zaidi ya 1,000 kutoka nchi zaidi ya 50, huku yakiwa na shughuli kama vile utoaji kwa umma bidhaa mpya, mhadhara wa kitaalamu na kujenga uhusiano wa kibiashara.
Yakiwa na eneo la maonyesho lenye ukubwa wa mita za mraba zaidi ya 45,000, maonyesho hayo yanaonesha aiskrimu na vitu vyake vya kuiandaa, pamoja na vifaa vya friji na mashine zingine.
Zhang Xiaohong, mkuu wa kamati ya maandalizi ya maonyesho hayo, amesema maonyesho hayo yanaonyesha uhai wa sekta ya aiskrimu ya China na mwelekeo mpya katika soko kubwa, kama vile kuongezeka kwa uelewa wa ulinzi wa afya na mazingira.
Albert Vega Duran anayefanya kazi katika Kampuni ya IBK Tropic, muuzaji wa vitu vya kuchanganywa kwenye aiskrimu kutoka Hispania ambaye amekuwa akionyesha bidhaa katika maonyesho hayo kwa zaidi ya miaka 10, amesema kuwa China ni mzalishaji mkubwa na mtumiaji wa aiskrimu na bado ina uwezo wa kukua.
"Tunatembelea maonyesho haya kukutana na wateja na kupata oda zaidi. Tunajaribu kuboresha bidhaa zetu," amesema Duran.
Yakiwa yalianza kufanyika tangu Mwaka 1998, Maonyesho hayo yamehimiza mawasiliano ya kimataifa ndani ya sekta ya aiskrimu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma