Mashindano ya Ustadi wa Kupika Chakula cha Baharini kwa miji ya pwani ya China 2024 yafanyika (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 29, 2024
Mashindano ya Ustadi wa Kupika Chakula cha Baharini kwa miji ya pwani ya China 2024 yafanyika
Chakula kinachoitwa “You Long Si Hai”. (Picha na Lei Qijun/People’s Daily Online)

Mashindano ya Kitaifa ya Ustadi wa Kupika Chakula cha Baharini kwa miji ya pwani ya China 2024 yamefanyika katika Mji wa Beihai, Guangxi, China, Septemba 26 ambapo wanataaluma wapishi zaidi ya 110 wameshindana kupika, na vyakula maalum zaidi ya 200 vimeshindana kwa kuandaliwa vema.

Wu Dongdong, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wapishi wa Guangxi ameujulisha umma kuwa, mashindano hayo yamehusisha sehemu mbili, ambazo ni kupika kwa kutumia vitu vilivyochaguliwa tayari, na kupika kwa kutumia vitu vilivyochaguliwa na wapishi wenyewe. Kati yake, vyakula vilivyopikwa kwa kutumia vitu vilivyochaguliwa tayari lazima vitumie vitu vya chakula cha baharini kilichoandaliwa maalum na kamati ya maandalizi, ambacho ni duvi za Beihai.

Baada ya mashindano makali ya mtandaoni na ukumbini, washindi 12 wa tuzo ya kwanza, washindi 36 wa tuzo ya pili na washindi 58 wa tuzo ya tatu walichaguliwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha