Sekta ya utengenezaji tiara yastawi katika Mji wa Weifang, Shandong, Mashariki mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 15, 2024
Sekta ya utengenezaji tiara yastawi katika Mji wa Weifang, Shandong, Mashariki mwa China
Bidhaa za utamaduni zenye ubunifu na kauli mbiu ya tiara zikionekana katika picha kwenye karakana ya tiara iliyoko Wilaya ya Hanting ya Mji wa Weifang, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, Oktoba 14, 2024. (Xinhua/Xu Suhui)

Utamaduni wa tiara na viwanda vinavyostawi vya utengenezaji wa tiara katika Mji wa Weifang, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China una historia ndefu na tajiri. Mwaka 2006, ustadi wa utengenezaji wa tiara wa mji huo wa Weifang uliorodheshwa kwenye vitu vya urithi wa utamaduni usioshikika wa kitaifa.

Kwa sasa, mji huo wa Weifang viwanda zaidi ya 600 vya kutengeneza tiara, huku thamani yao ya uzalishaji wa kila mwaka ikizidi yuan bilioni 2 (sawa na dola za Kimarekani milioni 280) na bidhaa zao zikiuzwa kwa nchi na maeneo zaidi 50. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha