

Lugha Nyingine
Meli Hospitali ya Kikosi cha Majini cha China“Peace Ark” yamaliza ziara nchini Cameroon na kuelekea Benin (4)
![]() |
Meli Hospitali ya Kikosi cha Majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) “Peace Ark” ikitoa huduma za matibabu na madaktari kusambaza vipeperushi nchini Cameroon, Tarehe 10, Oktoba. (Xinhua/Liu Zhilei) |
Meli hospitali ya kikosi cha majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), “Peace Ark”, ambayo ilikuwa ikitekeleza “Jukumu la Mapatano 2024”, imeondoka kwenye Bandari ya Douala Oktoba 14, ikimaliza kwa mafanikio ziara yake ya kwanza nchini Cameroon, na kuelekea Benin, kituo chake cha kumi cha majukumu.
Katika ziara yake hiyo ya kirafiki ya siku saba, meli hiyo hospitali imetoa huduma za matibabu kwa watu zaidi ya 6800 na kufanya uchunguzi na upimaji kwa watu karibu 3,000 hali ambayo imepokelewa kwa furaha na kusifiwa na watu wa Cameroon.
Mbali na huduma ya matibabu kwenye meli, meli hiyo pia ilipeleka timu kadhaa zikiwemo za madaktari kwenye hospitali na majeshi za huko kutoa huduma za pamoja za afya, mabadilishano ya kitaaluma, mafunzo ya ujuzi wa hudumam ya kwanza na shughuli nyinginezo, ikiendeleza kikamilifu mabadilishano na ushirikiano kati ya China na Cameroon katika nyanja ya afya.
Zaidi ya hayo, wawakilishi wa wanajeshi hao wa China pia walienda Chuo Kikuu cha Douala kufanya mihadhara ya maarifa ya afya na mawasiliano ya kitamaduni, na kucheza mechi ya kirafiki ya mpira wa miguu na maofisa na wanajeshi wa Cameroon, ambayo imeimarisha zaidi maelewano na kuzidisha urafiki kati ya pande hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma