

Lugha Nyingine
Barabara Kuu Mpya kuleta urahisi kwa watalii kufika Bonde la Jiuzhai katika Mkoa wa Sichuan, China
Baada ya kufunguliwa kwa barabara kuu ya Jiuzhaigou-Mianyang katika Mkoa wa Sichuan, kusini-magharibi mwa China, muda wa kusafiri kutoka Chengdu, mji mkuu wa mkoa huo hadi Wilaya ya Jiuzhaigou lilipo Bonde maarufu la Jiuzhai utafupishwa kutoka saa nane za awali hadi saa nne. Bonde la Jiuzhai, ambalo pia linajulikana kwa jina la Bustani ya Taifa ya Jiuzhaigou ya China, linajulikana sana kwa maporomoko yake ya maji ya kuvutia, misitu minene ya kijani, maziwa ya nyanda za juu, na uumbikaji wa miamba ya karst.
Kuzinduliwa kwa sehemu mpya ya reli ya Sichuan-Qinghai na barabara kuu inayotarajiwa kukamilika kujengwa hivi karibuni ya Jiuzhaigou-Mianyang kutawezesha watalii kufika Bonde la Jiuzhai, ikiifanya Wilaya ya Jiuzhaigou kuharakisha kusonga mbele kujiunga katika mzunguko wa kiuchumi wa Chengdu-Chongqing.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma