Wanariadha wa Ethiopia washinda mbio za Marathon za Amsterdam

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 22, 2024
Wanariadha wa Ethiopia washinda mbio za Marathon za Amsterdam
Yalemzerf Yehualaw wa Ethiopia akishangilia kwenye jukwaa la kutoa medali baada ya kushinda mbio za wanawake kwenye mashindano ya 48 ya mbio za Marathoni za Amsterdam yaliyofanyika Amsterdam, Uholanzi, Oktoba 20, 2024. (Picha na Sylvia Lederer/Xinhua)

THE HAGUE - Wanariadha wa Ethiopia Tsegaye Getachew na Yalemzerf Yehualaw wameshinda mbio za Marathon za Amsterdam kwa wanaume na wanawake mtawalia siku ya Jumapili ambapo Getachew amepata ushindi wake wa pili wa mbio hizo za marathon kwa kukimbia kwa muda wa saa 2:05:38.

Licha ya kukaribia kujichanganya ambapo alikaribia kukosea sehemu ya kugeukia mara tu kabla ya kuingia kwenye Uwanja wa Olimpiki, alirekebisha haraka makosa yake. Nyuma yake kwa karibu walikuwa ni mwanariadha mwenzake wa Ethiopia Boki Asefa, aliyemaliza katika nafasi ya pili kwa kukimbia kwa muda wa saa 2:05:40, na wa Israeli Maru Teferi, aliyeibuka wa tatu kwa kukimbia kwa saa 2:05:42.

Katika mbio za wanawake, Yalemzerf Yehualaw aliweka rekodi mpya ya kozi, akishinda kwa kukimbia kwa muda wa saa 2:16:52. Mwanariada mwenzake wa Ethiopia Haven Hailu alifuata katika nafasi ya pili kwa kukimbia kwa muda wa saa 2:19:29, huku Winfridah Moseti wa Kenya akichukua nafasi ya tatu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Deng Jie)

Picha