Maonyesho ya 7 ya Sauti Duniani yaanza mjini Hefei, mashariki mwa China (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 25, 2024
Maonyesho ya 7 ya Sauti Duniani yaanza mjini Hefei, mashariki mwa China
Watembeleaji wakitazama roboti mbwa kwenye Maonesho ya 7 ya Sauti Duniani, Oktoba 24.

Maonyesho ya 7 ya Sauti Duniani na Gulio la Wabunifu wa Programu za Kompyuta 1024 la iFlytek Mwaka 2024 yameanza mjini Hefei, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China, Alhamisi, Oktoba 24.

Maonyesho hayo ya mwaka huu yatafanyika kwa siku nne, yakiwa na shughuli ya Maonyesho ya Bidhaa za Ubunifu wa Akili Mnemba katika wakati huohuo, pamoja na kumbi nane za maonyesho zenye mada mahsusi kama vile sayansi na teknolojia, viwanda, elimu, maisha na nyinginezo.

Teknolojia na bidhaa za kisasa zinaonyeshwa kwenye maonyesho hayo, zikivutia watembeleaji wengi kwenda kujionea na kuelewa matumizi ya Akili Mnemba katika viwanda, elimu, starehe na burudani.

(Xinhua/Picha na Fu Tian)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha