

Lugha Nyingine
Kituo cha Vipaji cha Asia Kaskazini Mashariki (Shenyang) chazinduliwa
Mkutano wa Mabadilishano ya Vipaji wa Asia Kaskazini Mashariki (Shenyang) na Mkutano wa Uendelezaji wa Kampuni Tarajiwa Adimu za Thamani za China (Unicorn companies) umefanyika huko Shenyang, Mkoa wa Liaoning wa China, siku ya Alhamisi, Oktoba 24.
Katika mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu wa Kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ya Mji wa Shenyang Wang Yongwei, mjumbe wa kudumu wa Kamati ya CPC ya Shenyang ambaye pia ni Naibu Meya wa Shenyang, Wu Tingbao, Mkuu wa People’s Daily Online ambaye pia ni Mkurugenzi wa Maabara Muhimu ya Kitaifa ya Utambuzi wa Maudhui ya Mawasiliano ya Habari Ye Zhenzhen, pamoja na Naibu Katibu wa Kamati ya CPC ya People’s Daily Online, Zhang Feng, kwa pamoja walizindua Kituo cha Vipaji cha Asia Kaskazini Mashariki (Shenyang).
Kituo hicho kimeanzishwa kwa pamoja na Ofisi ya Oganaizesheni ya Kamati ya CPC ya Mji wa Shenyang, Idara ya Rasilimali Watu na Hifadhi ya Jamii ya Shenyang, pamoja na People’s Daily Online, kikiwa ni mfumo unganishi wa ushirikiano wa idara mbalimbaili kufanya kazi nzuri ya kuvutia vipaji na pia ni chapa kuu ya kueneza sera za vipaji za Shenyang.
Kituo hicho kitajumuisha pamoja kazi mbalimbali kama vile huduma ya maelekezo ya serikali, utoaji nafasi za kazi za kampuni mbalimbali, mafunzo kwa vipaji vya vyuo vikuu, uungaji mkono wa kifedha na uenezaji na utangazaji matangazo wa vyombo vya habari, na kujenga jukwaa la ushirikiano wa kazi ya vipaji lenye makao yake katika Mkoa wa Liaoning, ambalo linalenga eneo la Kaskazini Mashariki mwa China, na kuunganisha kazi za vipaji za Asia Kaskazini Mashariki.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma