Lugha Nyingine
China yatangaza wanaanga wa Chombo cha Shenzhou-19 (5)
JIUQUAN - Shirika la Anga ya Juu la China leo Jumanne limetangaza kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa wanaanga wa China Cai Xuzhe, Song Lingdong na Wang Haoze watatekeleza majukumu kwenye chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-19, Cai atakuwa mkuu wa wanaanga hao.
Msemaji wa shirika hilo Lin Xiqiang, amesema chombo hicho kimepangwa kurushwa saa 10:27 alfajiri kesho Jumatano (Kwa saa za Beijing) kutoka Kituo cha Kurushia Satalaiti cha Jiuquan, Kaskazini Magharibi mwa China.
Bw. Cai alikamilisha majukumu kwenye chombo cha Shenzhou-14 Mwaka 2022. Song na Wang, miongoni mwa kundi la tatu la wanaanga wa China, watakuwa kwenye majukumu hayo kwa mara ya kwanza, wote wawili walizaliwa kwenye miaka ya 1990.
Song ni alikuwa rubani wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), na Wang alikuwa mhandisi mkuu katika Akademia ya Teknolojia ya Uendeshaji Vyombo vya Anga ya Juu ya China.
Kwa sasa Wang ni mhandisi pekee wa kike wa anga ya juu na atakuwa mwanamke wa tatu wa China kutekeleza majukumu kwenye chombo cha anga ya juu.
Kazi ya utafiti wa kisayansi wa fani mbalimbali yakamilika mkoani Xinjiang, China
Mandhari ya majira ya mpukutiko ya Hifadhi ya Taifa ya Ardhi Oevu ya Huaxi huko Guiyang, China
Barabara Kuu ya Jianhe-Liping yafunguliwa kwa matumizi ya umma kusini magharibi mwa China
Wanariadha wa Ethiopia washinda mbio za Marathon za Amsterdam
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma