China yarusha chombo chenye wanaanga cha Shenzhou-19 kwenda anga ya juu (8)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 30, 2024
China yarusha chombo chenye wanaanga cha Shenzhou-19 kwenda anga ya juu
Chombo cha Shenzhou-19 cha kupeleka wanaanga kwenye anga ya juu, kikiwa juu ya roketi ya Long March-2F, kikirushwa kutoka Kituo cha Kurushia Satalaiti cha Jiuquan kilicho kaskazini-magharibi mwa China, Oktoba 30, 2024. (Wang Jiangbo/Xinhua)

JIUQUAN - China imerusha chombo cha Shenzhou-19 cha kubeba wanaanga kwenye anga ya juu siku ya Jumatano, ambacho kitapeleka wanaanga watatu kwenye kituo cha China cha anga ya juu kinachozunguka kwenye obiti, ili wafanye majukumu ya miezi sita. Wanaanga hao ni pamoja na mwanamke wa kwanza mhandisi wa mambo ya anga.

Chombo hicho, kilichokuwa juu ya roketi ya kubeba ya Long March-2F, kimerushwa kutoka kwenye Kituo cha Kurushia Satalaiti cha Jiuquan kilichoko kaskazini magharibi mwa China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha