Lugha Nyingine
Uturuki yaadhimisha miaka 101 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Uturuki (2)
Watu wakisherehekea maadhimisho ya miaka 101 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Uturuki mjini Istanbul, Uturuki, tarehe 29 Oktoba 2024. (Picha/VCG) |
ISTANBUL – Uturuki imesherehekea maadhimisho ya miaka 101 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Uturuki jana Jumanne kwa kufanya shughuli na kumbukumbu tofauti kote nchini humo ambapo mjini Ankara, Rais Recep Tayyip Erdogan na maafisa wengine wa serikali waliweka mashada ya maua kwenye Jumba la Anitkabir, kaburi la Mustafa Kemal Ataturk, mwasisi wa jamhuri hiyo.
Katika ujumbe wake wa siku hiyo ya taifa, Rais Erdogan amesema serikali yake "itashikilia kwa uthabiti zaidi mtazamo wa historia na maadili ya ustaarabu wa taifa ili kuimarisha amani, utulivu, usalama na haki ndani ya nchi, katika kanda na duniani kote."
Sherehe zimefanyika siku nzima mjini Istanbul, zikipambwa na gwaride, shughuli za ukumbusho na hotuba zilizojikita katika shambulizi la hivi karibuni la kigaidi mjini Ankara huku zikienzi uhimilivu wa taifa na wale waliopoteza maisha.
"Tutazuia ujanja wa wale wanaoshambulia nchi yetu na amani yetu, na tutajenga Karne ya Baadaye," Gavana wa Istanbul Davut Gul amesema kwenye hafla ya gwaride la kijeshi.
Miongoni mwa mambo muhimu katika sherehe hizo ni Mbio za 5 za Kimataifa za Boti, zilizoandaliwa na Ikulu ya Uturuki, zilizofanyika nje ya Jumba la Dolmabahce kwenye Mlango-Bahari wa Bosphorus, eneo ambalo lina umuhimu wa kihistoria ambako Ataturk aliaga dunia.
Kazi ya utafiti wa kisayansi wa fani mbalimbali yakamilika mkoani Xinjiang, China
Mandhari ya majira ya mpukutiko ya Hifadhi ya Taifa ya Ardhi Oevu ya Huaxi huko Guiyang, China
Barabara Kuu ya Jianhe-Liping yafunguliwa kwa matumizi ya umma kusini magharibi mwa China
Wanariadha wa Ethiopia washinda mbio za Marathon za Amsterdam
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma