Lugha Nyingine
Wanaanga wa China wa chombo cha Shenzhou-19 waingia kwenye kituo cha anga ya juu (5)
Picha hii iliyopigwa katika Kituo cha Udhibiti wa Anga cha Beijing Oktoba 30, 2024 ikionyesha wanaanga wa vyombo vya anga ya juu vya Shenzhou-18 na Shenzhou-19 wakifanya mazungumzo. (Han Qiyang/Xinhua) |
BEIJING - Wanaanga watatu wa chombo cha Shenzhou-19 cha China wameingia kwenye kituo cha anga ya juu cha China cha Tiangong na kukutana na wanaanga wengine watatu siku ya Jumatano, wakianzisha raundi mpya ya makabidhiano ya wanaanga kwenye obiti.
Wanaanga wa chombo cha Shenzhou-18 walifungua lango la kituo hicho majira ya 6:51 Mchana (Saa za Beijing) na kukaribisha wanaanga hao wapya waliowasili, kwa mujibu wa Shirika la Anga ya Juu la China (CMSA).
Wanaanga hao sita kisha wakapiga picha za pamoja kwa ajili ya makumbusho hayo ya kukutana kwa mara ya tano kwa wanaanga wa China kwenye anga ya juu katika historia ya anga ya juu ya China.
Wataishi na kufanya kazi pamoja kwa siku takriban tano kukamilisha kazi zilizopangwa na kazi ya makabidhiano, CMSA imesema.
Wanaanga hao wa chombo cha Shenzhou-18 wamepangwa kurejea duniani kwenye eneo la kutua la Dongfeng, Kaskazini mwa China Novemba 4.
Kazi ya utafiti wa kisayansi wa fani mbalimbali yakamilika mkoani Xinjiang, China
Mandhari ya majira ya mpukutiko ya Hifadhi ya Taifa ya Ardhi Oevu ya Huaxi huko Guiyang, China
Barabara Kuu ya Jianhe-Liping yafunguliwa kwa matumizi ya umma kusini magharibi mwa China
Wanariadha wa Ethiopia washinda mbio za Marathon za Amsterdam
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma